Picha hizo za video ambazo zilionyeshwa katika kipindi cha ukweli halisia cha rapa huyo ambacho kinafahamika kwa jina la T.I.'s Road To Redemption zinasemekana kuwaumiza mno wana familia wa kijana Joseph William ambapo uchukuaji wa picha hizo umefanyika february 2009 katika kipindi cha mazishi yake.
wanafamilia hao walitinga kwa mabosi wa MTV na kuelezea ni jinsi gani waliumizwa na rapa huyo kumwita mtoto wao "hustler" na kuzitumia picha za mwili wake kuzionyesha katika kipindi hicho bila ridhaa yao, na kwamba wamepanga kumlipisha fidia T.I kwa kufanya kitendo kinachoamsha msongo wa mawazo kwao.
