Tuesday, March 22, 2011

WANAMUZIKI 12 WA KUNDI LA 5 STAR MODERN TAARAB WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

Mashabiki wa kundi la 5 stars modern taarab na watanzania kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo walipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali mbaya ya gari iliyosababisha vifo vya wanamuziki 12 wa kundi hilo.
Ajali hiyo ambayo ilitokea katika barabara yairinga katika hifadhi za wanyama za  Mikumi mkoani morogoro majira ya saa mbili usiku.
Mavuvuzela inatoa mkono wa pole kwa wanafamilia wote waliopoteza ndugu zao ktk ajali hiyo, na inawaombea majeruhi wapone haraka
Mungu Azilaze Roho Za Marehemu Mahala Pema Peponi Aamin...