Thursday, May 19, 2011

NILIKUA NA NDOTO ZA KUA MISS TANZANIA-baby J

Mwanadada machachari katika fani ya muziki wa Bongoflava nchini Tanzania Jamila Maria Abdallah (Baby J) kutoka visiwani Zanzibar amesema kwamba kuna kipindi fulani katika maisha yake alitamani kua mrembo atakae iwakilisha tanzania katika mashindano ya dunia, lakini ndoto zake zilikufa ghafla baada ya kubaini vijimambo fulani ambavyo havikumpendeza katika fani hiyo ''nilikua chini ya uongozi wa wakina mama fulani hapa bongo ambao walishaanza kuniandaa na Miss vitongoji na wilaya, lakini kabla sijagusa kambi yoyote nikabaini tabia chafu katika fani hiyo, ila siwashauri wale wenye ndoto za kuwa warembo wasijiingize kwani wapo warembo wenye tabia safi tu'' alisema black beauty huyo