Thursday, May 19, 2011

TUNAGOMBANA SANA ILA MUZIKI UNATUPATANISHA- Jay20

Mwanamuziki anaegombani tuzo ya mwanamuziki bora ambae ametangaza muziki wa kizazi kipya wa Zanzibar Kimataifa kwa mwaka 2010-2011 Juma alkalass Tumba (Jay20) amesema kwamba amekua akigombana sana na mpenzi wake (hakumtaja jina) kuhusiana na masuala ya muziki wake lakini hatimae muziki huo huo huwapatanisha
''katika maisha ya kawaida unaweza kukutana na mambo mengi lakini cha muhimu zaidi katika masuala ya mapenzi na career ya mtu, ni kupata mwenza ambae atakua anakukosoa kosoa, hata kama itauma, mwisho wa siku atakuambia jambo linalofurahisha na ukajikuta unafikiria vitu viwili kwa wakati mmoja, mapenzi na muziki, nampenda mpenzi wangu, napenda muziki wangu'' alisema mkali huyo