Mshindi wa tunzo Moja ya kilimanjaro Music awards kwa mwaka uliopita A.T amesema kwamba wimbo wake mpya wa Nyangumi ambao ameuachia hivi karibuni unawalenga watu flani ambao hapo awali walikua ni watu wa karibu sana kwake, akiongea na mavuvuzela, At amesema kwamba ni ngumu kuishi na watu ambao wao wanataka wakutawale kimaamuzi kila kukicha na ndio sababu ya yeye kuachia wimbo huo akijiita Nyangumi (kiumbe kikubwa cha baharini chenye kupenda raha)
watu wakaribu wameuelezea wimbo huo kama jibu kwa offside trick kwa ule wimbo wa "kidudu mtu" ambao inasemekana ulimlenga yeye.
