Sunday, April 3, 2011

NICKY MINAJ NA USHER WAVUMISHIWA KUPIGA TAFU UJIO MPYA WA BRITNEY

Tokea mwanamuziki Enrique Iglessia akane kwamba hatokuwepo katika Ufunguzi wa Kumkaribisha tena Britney katika game ya Muziki,tetesi zimeanza kuvuma juu ya nani atachukua nafasi yake ingawa hapo hapo inaelezwa kwamba Billboard wametoa tamko kwamba Iglessias yupo katika gati gati ya kufanya tour hiyo kama ilivyopangwa, ni kama vile Britney yupo katika mchakato wa kutafuta majina makubwa ya kuweza kumpiga tafu.
katika interview aliyofanya na MTV mwanadada Britney alimuorodhesha Usher kwamba ndie mwanamuziki anaetaka kuzunguka nae ktk tour hiyo kwa vile brazameni huyo yupo juu kwa sasa.
hata hivyo wataalamu wa masuala ya burudani wanasema kwamba hii si dalili nzuri kwa tour za Britney, kwa sababu brazameni Usher yupo bize na miradi yake na iwapo atakubali dili hilo basi itakua ni kwa ajili ya ufunguzi wa au kichwa cha habari tu na si kuzunguka ulimwengu mzima.
kulingana na TMZ inaonekana kama kwamba Nick Minaj ndie pendekezo kubwa zaidi katika tour hiyo baada ya wakali hao kuonekana kusua sua,
Mwanasheria wa Nicky pamoja na wa Britney wapo katika maongezi serious kwa ajili ya tour hiyo, na tamko la mwisho linatazamiwa kutolewa siku chache zijazo