Sunday, April 3, 2011

CHRIS BROWN AFANYA MTAFARUKU BAADA YA KUULIZWA SUALI KUHUSU RIHANNA

Mkali wa rnb kutoka pande za U.S.A Chris Brown aliamua kusitisha ghafla interview yake wakati akihojiwa katika kipindi cha tv cha Good Morning America baada ya hoster wa kipindi hicho kumuuliza suali kuhusu Rihanna.
sharo baro huyo ambae awali inaripotiwa kwamba alikataa kata kata kuulizwa suali lolote linalohusiana na sista duu Rihanna wakati producer wa show hiyo alipomfata backstage kumtaarifu juu ya masuali ambayo angeulizwa akiwa on air.
Mwanamuziki huyo kuanza kipindi alikua akiongea kwa sauti ya juu huku akirusha viti na kumchimba mikwala producer huyo kwamba asijaribu kumuuliza chochote kuhusiana na Rihanna, hata ikafikia kuomba walinzi waende chumba chake cha kubadilishia nguo kwa madai ya kwamba anafanyiwa fujo.
Wakati anafanya mahojiano hewani, hoster wa shoo hakutii amri ya Chris brown pengine bila kujua akamuuliza suali kuhusiana na kumdhalilisha rihanna mwaka 2009, hali iliyomfanya mwanamuziki huyo kunyanyuka ghafla na kuondoka mbele ya watizamaji na kuelekea nyuma ya mlango wa kutokea katika jengo hilo.
Chris brown ambae kwa sasa amekwabua nywele zake na kuzifanya blond, alivua t shirt yake na kumtupia mlinzi wa jengo hilo na kutokomea mitaa ya manhattan huku akifuatiliwa karibu na walinzi wake