Mwanadada machachari ktk fani ya muziki wa Bongo flava Nchini Tanzania Jamila Maria Abdalla (Baby jay) amesema kwamba hafikirii kujiunga na kikundi chochoto cha taarab kama vile wengi wanavyofikiria kumshauri.
Akiteta na Mavuvuzela baby jay amesema kwamba, anadhani swaga zake ni za Kizazi kipya zaidi, na watu wakimuona kwamba ameshiriki katika taarab au miduara wajue kwamba itakua ni kwa kupendekezwa tu.
