MICHAEL JACKSON ALIKUA AMEFULIA- DOKTA MURRAY
Kesi inayomkabili Dakitari ambae amebebeshwa msala wa kusababisha Kifo cha Mfalme wa Pop Duniani (Michael Jackson) imenguruma tena wiki hii, ambapo Dr. huyo anaefahamika kwa jina la Conrad Murray ameiambia mahakama inayosikiliza kesi hiyo kwamba Jackson alijiua mwenyewe kwa kutaka ampige over dose ya "powerful sedative Propofol" kwa kua mfalme huyo alikua katika dimbwi kubwa la msongo wa mawazo yaliyotokana na Madeni makubwa, na mipango ya show yake ya mwisho ambayo alipanga kuifanya jijini London.