Katika hali ya kushtusha mtangazaji wa times f.m Dida (dida wa mchops) amewapiga dongo la wazi viongozi wa kundi la 5stars modern taarabu ambalo wasanii wake 13 walipoteza maisha kutokana na ajali mbaya ya gari kwamba hawajui wema wala shukurani.
akiongea kupitia kipindi cha mitikisiko ya pwani dida alisema "sisi kama times kama kusikitika tumeshasikitika, hatuna haja ya kupewa shukurani na wao kwani wema wetu tayari unajuulikana kitambo, lakini kitendo chao cha kukitaja kituo kimoja tu cha redio kwamba ndio wanakishukuru kwa kuripoti tukio zima la msiba wao si cha kiungwana, si bora wangelitaja vituo vyote vya Tanzania? na uongozi wa times fm tunawaambia kwamba sisi tupo, kama hawatokuja kwa bajaji watakuja na ndala zao," alipasha Mtangazaji huyo Baada ya kukerwa na tukio hilo lililotolea katika arobaini ya kuwaombea marehemu hao.