Friday, April 29, 2011

PRINCE CHARLES NA KATE WAVUNJA SHERIA ZA KI FALME

Harusi Ya Kifalme Ambayo ni Kubwa kuliko hata ile ya Princess Diana imemaliza Siku ya leo (Ijumaa) huku ikiacha Gumzo kubwa ulimwenguni baada ya maharusi wa ndoa hiyo kufuata nyayo zile zile za wakina Princess Diana na Prince charles  za Kupigana Busu Hadharani.
Prince William na Mchumba wake Kate Middelton wamemaliza harakati zote za kufanikisha ndoa yao, ambapo walifunga ndoa hiyo katika balcon za kasri la Bukingham huku wakishuhudiwa na wageni waalikwa milioni mbili.(ukiachilia mbali mabilioni waliokua wakifatilia kupitia screen na televisheni duniani kote)
mengi yalikua yakizungumzwa tokea engegment ya wawili hao hadi ndoa yao.
mavazi ya wanandoa hao pamoja na wasimamizi wao yalikua gumzo tosha ambapo vito vya thamani kubwa sana vilitumika.
miongoni mwa wageni waalikwa wa shughuli hiyo alikua ni mfalme mswati wa swaziland...nchi ambayo inasemekana kwamba wawili hao walikutana walipokua wakifanya utalii na huenda wakafanyia fungate yao.
farasi wapatao mia walilifuata ringsho la bibi na bwana harusi hadi nje ya kasri hilo ambapo wawili hao uvumilivu uliwashinda na kuamua kupigana busu la haraka haraka (kitendo ambacho kawaida hufanyika katika balconi kwa wanandoa wa kawaida)
kwa mara ya kwanza katika ndoa za kifalme za ukoo huo Diana na Charles ndio walipigana busu hadharani na ndoa yao ikavunjika miaka michache baadae, lakini kwa siku ya leo kila mtu aliwatakia wawili hao maisha ya furaha!
miongoni mwa wageni waliopigiwa nderemo na vifijo walipokua wakiwasili katika harusi hiyo ni rafiki wa karibu wa familia ya kifalme mwanamuziki shoga elton john ambae aliwasili katika kasri hilo akiwa na bwana wake huku wamekamatana mikono!!
hata hivyo, rais wa marekani Barak Obama pamoja na waziri mkuu wa uingereza hawakualikwa harusi hiyo kutokana na kile ambacho familia hiyo walikiita '''Ni harusi ya Kifamilia sio ya kisiasa wala kiserekali'